PROMOSHENI ZA WIKI Y...
PROMOSHENI ZA WIKI YA MAJI MACHI, 2023
16 Mar, 2023

PROMOSHENI ZA WIKI YA MAJI MACHI, 2023

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TABORA KUELEKEA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI TAREHE 16 HADI 22 MACHI 2023 YENYE KAULI MBIU:-

“KUONGEZA KASI YA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA MAJI KWA MAENDELEO ENDELEVU YA UCHUMI”

IMEANDAA PROMOSHENI KABAMBE KWA WAKAZI WA MANISPAA YA TABORA KAMA IFUATAVYO;-

  1. WATEJA WAPYA
  • WATALIPIA SHILINGI 150,000/= KWA MKUPUO
  • MAUNGANISHO YATAFANYWA NDANI YA SIKU 7 ZA KAZI.
  • WAKAZI WATAKAOHUSIKA NI WOTE WALIOPO UMBALI WA MITA 5 HADI 50 KUTOKA KWENYE BOMBA KUBWA LA MAJI
  • MTEJA ATALIPIA HUDUMA BAADA YA KUPIMIWA NA KUKIDHI SHARTI LA UMBALI WA MITA ZISIZOZIDI 50.

 

  1. WATEJA WALIOKATIWA MAJI KUANZIA JUNI 2022 KURUDI NYUMA.
  • MTEJA HATALIPA GHARAMA YA KUREJESHA MAJI TSHS 15,000/=
  • MTEJA ATATAKIWA KULIPA NUSU YA DENI NA DENI LINALOBAKI LITALIPWA KWA AWAMU NNE HADI IFIKAPO JUNI 2023.
  • WATEJA WALIOKATIWA MAJI WENYE MIUNDOMBINU YA MAJI ILIYO HARIBIKA ISIYOZIDI UMBALI WA MITA 50 WATATAKIWA KULIPA 150,000/= TU NA KUWEKEWA MIUNDOMBINU MIPYA YA MAJI.

 

IFAHAMIKE KUWA, WATEJA WOTE WALIOKATIWA MAJI KWA SABABU YA KUBAINIKA KUTUMIA MAJI KINYUME NA TARATIBU HAWATAHUSIKA NA PROMOSHENI HII.

 

MWISHO WA PROMOSHENI HII NI TAREHE 15.04.2023

TUMIA FURSA MUDA NI MFUPI.

 

Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji - TUWASA