Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Ukiona bomba limepasuka maji yanamwagika unatakiwa kupiga namba ya bure ya TUWASA ambayo ni 0800780063 na kueleza taarifa ya eneo bomba lilipopasuka.
Bomba la Mteja linapopasuka mbele ya Mita ya Maji  mteja anawajibika kulitengeneza na kuzuia maji kumwagika lakini Bomba likipasuka nyuma ya Mita ya Maji TUWASA wanawajibu wa kulitengeneza 
Mteja wa Maji anawajibika kuilinda na kuhakikisha Mita ya Maji haiharibiwi wala kuibwa.
Utapata ujumbe mfupi wa Bili yako kila mwezi kuanzia Tarehe 16 kupitia simu yako ya Mkononi.
Unatakiwa kujaza Dodoso lenye Taarifa zako zote muhimu lililopo hapa kwenye Website yetu na kulituma TUWASA kisha utapimiwa eneo lako na kupewa hati ya madai  na kuunganishwa kwenye huduma.