MRADI WA MAJI MJINI...
MRADI WA MAJI MJINI KALIUA, WAZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
17 Sep, 2023
MRADI WA MAJI MJINI KALIUA, WAZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

Leo Tarehe 16.09.2023 Ndg. Abdalla Shaibu Kaim, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, amezindua  mradi wa usambazaji maji mjini Kaliua kata ya Kaliua Mashariki kitongoji cha Umoja wenye gharama ya shilingi milioni 503,112,445 zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji.

Eng. Mayunga Antony Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA amesoma taarifa ya mradi iliyoeleza kuwa mradi umekamilika na wananchi 84 wameungwa na kupata huduma ya majisafi na salama.

 Mradi huu umeongeza  uzalishaji kutoka asilimia 44 Hadi asilimia 50 sawa na kutoka Lita 516,000 hadi Lita 566,000 kwa siku na amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza ili kujiunga kwenye huduma ya maji.

Ndg.  Abdalla Shaibu Kaim, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amesema ameipokea taarifa ya mradi, amekagua, kutembelea na  ameridhika na utekelezaji wake ikiwepo uwepo wa nyaraka zote muhimu.

Amesema anaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa fedha za mradi huu na hasa Serikali ina lengo la kuhakikisha wananchi wanapata Majisafi na salama kwa kumtua mama ndoo kichwani.

Baada ya kuridhika na utekelezaji wa mradi huu Ndg. Abdalla Shaibu Kaim amezindua  mradi wa usambazaji maji Mjini Kaliua sambamba na kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira.

Mwisho Mhe. Aloyce A. Kwezi, mbunge wa Kaliua ameishukuru Serikali kwa kuleta mradi huu na pia mradi mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria, ambao utamaliza kabisa kero ya maji katika Mji wa Kaliua.

"Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa".