BODI YAFANYA KIKAO N...
BODI YAFANYA KIKAO NA WATUMISHI - TUWASA
10 Feb, 2023
BODI YAFANYA KIKAO NA WATUMISHI - TUWASA

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt. Rogath Mboya ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Ameongea na Watumishi wa TUWASA tarehe 31.01.2023 Katika Kikao cha Watumishi Wote na Bodi na Kuwataka Watumishi Kufanya yafuatayo.-

  1. Watumishi Wafanye Kazi Kwa Bidii na Umoja Kama Timu ya Ushindi.
  2. Watumishi Wazingatie Kuhudumia Wateja Kwa Good Customer Care Ili Kuwapa Huduma Wanayoitarajia Wateja.
  3. Kila Mtumishi Atimize Wajibu Wake na pia ajiulize amefanya nini Ili Kuboresha Mapato ya Taasisi Ambayo yataboresha Maslahi ya Mtumishi Pia.
  4. Watumishi Wasiweke Vinyongo, Wasafishe Mioyo Yaliyomo Machafu Yaondoke Na Kazi Iwe Moja tu.
  5. Kuhakikisha Tuwasa Inakuwa Bora Katika Utoaji wa Huduma ili kuongeza Mapato ambayo yataboresha pia Maslahi ya Mtumish.
  6.  Kama Mtumishi ana Kero Aiwasilishe Kwa Mkuu Wake wa Idara Ili Itatuliwe.

Alimalizia Kwa Kusema Bodi ya Wakurugenzi ni Sikivu na Inajali Maslahi ya Watumishi. Hivyo Watumishi Waendelee Kuleta Mikakati Mizuri Kupitia Menejimenti ili Kuhakikisha Malengo yote Tuliyojiwekea Yanafikiwa.

 

 

Mwenyekiti Wa Bodi Bw. Dick Mlimuka (Wa Kwanza Kutoka Kulia) Alisisitiza Watumishi Kufanya Kazi Kwa Bidii, Good Customer Care Kwa Wateja, Watumishi Waone Fahari Kufanya Kazi TUWASA Na Waisemee Vizuri.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji Eng. Mayunga Kashilimu (Wa Pili Kutoka Kulia) Alipokea Maelekezo yote Kwa Niaba ya Watumishi na Kuahidi Kufanyia Kazi.