BODI MPYA YA TUWASA...
BODI MPYA YA TUWASA YAKUTANA NA MENEJIMENTI YA TUWASA
22 Sep, 2023
BODI MPYA YA TUWASA YAKUTANA NA MENEJIMENTI YA TUWASA

Ndugu Dick Mlimuka Mwenyekiti wa Bodi ya TUWASA amefanya kikao kifupi kilichohusisha wajumbe wapya wa Bodi na Menejimenti ya TUWASA kwa lengo la kufahamiana na kuendelea na majukumu.

Pia Eng Mayunga  Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA ambaye ndiye katibu wa Bodi hii aliwakaribisha na kuwapongeza wajumbe na kisha akaeleza muundo wa Bodi kuwa unajumuisha Mwenyekiti wa Bodi, Katibu wa Bodi aambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA, Katibu tawala wa Mkoa wa Tabora, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora.

Pia, yupo mwakilishi wa Wizara ya maji, mwakilishi wa watumiaji wakubwa wa maji, mwakilishi wa wanawake, mwakilishi wa wafanyabiashara na mwakilishi wa waheshimiwa madiwani.

Sambamba na hivyo Dkt Rogath Mboya mjumbe wa Bodi ambaye ni Katibu tawala wa Mkoa wa Tabora aliwapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa na pia aliipongeza menejimenti ya TUWASA kwa kujitambua na kufanya majukumu kwa ufanisi na hata ukizingatia miradi ya maji ya TUWASA imefanya vizuri Sana wakati wa kupitiwa na kukaguliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, 2023 ndugu Abdalla Shaibu Kaim. Amesisitiza Bodi na Menejimenti kuendelea kushirikiana .

Mwisho kabisa mjumbe wa Bodi ambaye ni mwakilishi wa watumiaji wakubwa wa maji Kanali Lyoba amesema atasimamia vema kuhakikisha watumiaji wakubwa wa maji wanalipa bili zao kwa wakati ili TUWASA iweze kujiendesha vizuri.