MRADI WA MAJI WA MIJ...
MRADI WA MAJI WA MIJI 28 UMEANZA KUTEKELEZWA RASMI KATIKA MIJI YA SIKONGE, URAMBO NA KALIUA.
08 Sep, 2023
MRADI WA MAJI WA MIJI 28 UMEANZA KUTEKELEZWA RASMI KATIKA MIJI YA SIKONGE, URAMBO NA KALIUA.

Meneja mradi wa Maji wa Miji 28 kutoka Wizara ya Maji Eng. Edward Tindwa, ameeleza kwamba mradi huu umeanza kutekelezwa rasmi katika Miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua, ambapo pamoja na kazi zingine, ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa Lita milioni moja (Lita 1,000,000) umeanza katika Mji wa Sikonge.

Ameeleza kuwa mradi huu utapata maji kutoka Ziwa Victoria na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwaka 2025 na maji yatapatikana kwa asilimia 100 maeneo yote ya Sikonge, Kaliua na Urambo.