MRADI WA MAJI SIKONG...
MRADI WA MAJI SIKONGE WAZINDULIWA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023.
15 Sep, 2023
MRADI WA MAJI SIKONGE WAZINDULIWA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023.

Leo Tarehe 14.09.2023 Ndg. Abdalla Shaibu Kaim (wa kwanza kushoto) Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2023, amezindua mradi wa usambazaji maji wenye gharama ya shilingi milioni 484,844,536 zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji uliopo Sikonge ambao unanufaisha wakazi wa kata ya Sikonge na Misheni.

Ndg. Abdalla Shaibu Kaim Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huu kwa kuwa umefuata taratibu zote muhimu ikiwepo kufanya tathmini ya athari za kimazingira katika eneo la mradi na nyaraka zote za mradi zipo.

Aidha amewaeleza wananchi kuwa Serikali ina dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha wananchi wote wanapata majisafi na salama.

Mwisho kabisa mradi huu umezinduliwa rasmi na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2023 ndg. Abdallah Shaibu Kaim na kufurahi zaidi kwa kuwa mradi huu uliwekewa jiwe la msingi mwaka 2022 na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru.