WATUMISHI TUWASA WAS...
WATUMISHI TUWASA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEIMOSI 2022/23 SIKONGE
02 May, 2023
WATUMISHI TUWASA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEIMOSI 2022/23 SIKONGE

Katika MAADHIMISHO YA MEIMOSI, 2023 yaliyofanyika katika viwanja vya Tasaf mjini SIKONGE watumishi wa TUWASA wameshiriki kikamilifu katika maandamano ambayo yameanzia katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya SIKONGE hadi viwanjani hapo.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mhe. Balozi Dkt Batilda S. Buriani (Mwenye nguo nyekundu) Mkuu wa mkoa wa Tabora ambaye aliwakabidhi watumishi hodari zawadi zao wakiwepo watumishi wa TUWASA ambao ni Bw. Said Mrisho, Bi. Upendo Bagaya na Bw. Samson Nyatutu na amewataka kuendelea kuwa wachapa kazi.

 

HONGERA WAFANYAKAZI HODARI

Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TUWASA inawapongeza sana wafanyakazi hodari wa TUWASA kwa mwaka 2022/2023

Kutoka kushoto ni Bw. SAID MRISHO, Bi. UPENDO BAGAYA na Bw. SAMSON NYATUTU