MENEJIMENTI YA TUWAS...
MENEJIMENTI YA TUWASA IMESHIRIKI PAMOJA NA WATUMISHI WA RUWASA NZEGA KATIKA SHUGHULI YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA KIGANDU NZEGA.
19 Sep, 2023
MENEJIMENTI YA TUWASA IMESHIRIKI PAMOJA NA WATUMISHI WA RUWASA NZEGA KATIKA SHUGHULI YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA KIGANDU NZEGA.

Leo Tarehe 19.09.2023 Menejimenti ya TUWASA imeshiriki pamoja na watumishi wa RUWASA Nzega katika shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji uliopo Kijiji cha Kigandu Nzega ikiwa ni utaratibu wa kushirikiana na kuboresha mahusiano baina ya TUWASA na RUWASA Tabora.

Uwekaji wa jiwe la msingi umefanywa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg. Abdalla Shaibu Kaim.

Mradi unathamani ya shilingi milioni 614,385,268 fedha iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameeleza Eng. Gaston R. Ntulo meneja RUWASA Nzega aliposoma taarifa ya mradi.

Aidha Eng. Gaston R. Ntulo ameendelea kueleza kuwa mradi umetekelezwa kwa asilimia 65, utakamika Octoba, 2023 na wananchi zaidi ya 6462 watahudumiwa kupitia chombo Cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii CBWSO ya MWAKASHANHALA.

Ndg. Abdalla Shaibu Kaim Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amesema amekagua, kutembelea na ameridhika na utekelezaji wa mradi huu na ameweka jiwe la msingi. Amesisitiza mradi ukamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.

"Tunza Mazingira Okoa Vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa".