MRADI WA MAJI KATA Y...
MRADI WA MAJI KATA YA NTALIKWA MANISPAA YA TABORA WAZINDULIWA RASMI NA MBIO ZA MWENGE.
15 Sep, 2023
MRADI WA MAJI KATA YA NTALIKWA MANISPAA YA TABORA WAZINDULIWA RASMI NA MBIO ZA MWENGE.

Leo Tarehe 15.09.2023 Ndg. Abdalla Shaibu Kaim Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, ameweka jiwe la Msingi katika mradi wa usambazaji maji wenye gharama ya shilingi milioni 601,868,971 zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji uliopo kata ya Ntalikwa, Manispaa ya Tabora ambao umetekelezwa kwa asilimia 58.5 hadi sasa.

Eng. Mayunga Antony Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA amesoma taarifa ya mradi iliyoeleza kuwa kilomita 11.47 kati ya 23.16 zimelazwa na vituo 8 Kati ya 11 vimeungwa kwenye huduma ya maji na tayari wananchi wameanza kupata huduma ya majisafi na salama. Mradi huu utakapokamika utanufaisha wakaazi 4000 wanaoishi maeneo ambayo mradi huu unatekelezwa

Ndugu Abdalla Shaibu Kaim Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amesema ameipokea taarifa ya mradi na ameridhika na utekelezaji wake ikiwepo uwepo na nyaraka zote muhimu na kufanyika kwa tathmini ya Mazingira kutokana na mradi.

Baada ya kuridhika na utekelezaji wa mradi huu ndugu Abdallah Shaibu Kaim ameweka jiwe la Msingi katika mradi huu wa usambazaji maji Manispaa ya Tabora.

"Tunza Mazingira Okoa Vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa".