Bwawa la Igombe

Bwawa la Igombe:

Bwawa la Igombe ni mojawapo wa chanzo maji kwa mji wa Tabora; lilijengwa na kuanza kutumika mwaka 1958.  Liko kilomita 20 Kaskazini Magharibi mwa mji wa Tabora. Uwezo wa hifadhi ni takriban mita za ujazo Milioni 41 na kufunika eneo la kilomita za mraba 12 kwa kiwango kamili cha usambazaji (FSL), na limezungukwa na eneo la maji la 2560 km2. Kina cha hifadhi ya maji ni karibu mita 5.