Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora ina utaratibu maalum unaopaswa kufuatwa na wateja ambao watahitaji kuunganishiwa maji safi na huduma ya kuunganisha majitaka.
Utaratibu ni kama ifuatavyo; -
i. Unatakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka na picha moja (passport size) na jaza Fomu ya Maunganisho Mapya ya Maji.
ii. Baada ya kujaza fomu, wafanyakazi wanaohusika watamjulisha mteja siku ya kutembelea eneo/nyumba kwa ajili ya uchunguzi na kutathmini nyenzo zitakazotumika kuwasilisha huduma.
iii. Mteja atajulishwa kuhusu gharama ya kuunganisha maji kwa njia ya SMS ya Simu.
iv. Mteja ataunganishwa baada ya kulipa kupitia CONTROL NUMBER aliyopewa.
KUMBUKA: Gharama zote za kuunganisha maji zitalipwa kwa kutumia CONTROL NUMBER. Kwa msaada zaidi tunakuomba uje Ofisini kwetu Tafadhali.